COPA DEL REY 2014/2015:- Yaliyojiri Januari 15,2015 wakati Real Madrid akitolewa kwa bao 4-2 na Atletico sasa Kuvaana na FC Barcelona. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 16, 2015

COPA DEL REY 2014/2015:- Yaliyojiri Januari 15,2015 wakati Real Madrid akitolewa kwa bao 4-2 na Atletico sasa Kuvaana na FC Barcelona.

Timu ya Atletico Madrid imeibuka na magoli  2 huko Santiago Bernabeu katika Dabi ya Jiji la Madrid ikiwa ni Marudiano ya raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya kuwania Kombe la Copa del Rey  na kumaliza mchezo dhidi ya Real Madrid  kwa sare ya bao 2-2 Usiku wa Januari 15,2015.


Hata hivyo, Atletico wanatinga Robo Faina Fainali kwa Jumla ya Bao 4-2 baada ya kushinda Mechi ya kwanza 2-0 Uwanjani kwao Vicente Calderon Wiki iliyopita.
Bao la kwanza la Atletico lilifungwa Dakika ya Kwanza tu na Real Madrid kusawazisha kupitia Sergio Ramos Dakika ya 20 na la Pili kwa Atletico lilifungwa tena Torres Dakika 1 tu tangu Kipindi cha Pili kuanza na Cristiano Ronaldo akaisawazishia Real Madrid.

Bila shaka kwenye Robo Fainali Atletico watakumbana na Barcelona ambao nao Usiku huo waliifunga  Ugenini  Elche bao 4-0 baada ya zile  5-0 katika Mechi yao ya kwanza.


Toni Kroos, Ronaldo, Sergio Ramos and James Rodriguez show off their awards before the Copa del Rey tie


ROBO FAINALI.

Januari 21 & 28,2015.

Malaga v Athletic Bilbao

Espanyol v Sevilla

Villareal v Getafe

Atletico Madrid v Barcelona

NUSU FAINALI.

Februari 11 & Machi 4,2015.

Malaga/Athletic Bilbao v Espanyol/Sevilla

Villareal/Getafe v Atletico Madrid /Barcelona

FAINALI

Mei 30,2015.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad