|
Katika
Mataifa yenye utamaduni wa kuongozwa na familia za kifalme au malkia Utawala wa
Malkia Elizabeth wa Uingereza ndio maarufu kuliko familia zote zinazoongoza.
Japo familia
hii ni maarufu lakini sio tajiri kama ambavyo watu wanaweza kudhani
wakilinganisha umaarufu na ukubwa wa nchi anayoiongoza, Malkia Elizabeth
na uwezo wa kifedha.
Familia ya
kifalme inayoongoza taifa la Lichtenstein ndio inayoongoza kwa utajiri
ikiwa na utajiri wa paundi bilioni 4.9.
Ikiongozwa
na Prince Hans-Adam II, familia hii ina utajiri ambao hauna uhusiano wowote na
kodi za wananchi wa taifa dogo la Lichtenstein na utajiri walio nao kina
Hans-Adam II unatokana na kampuni ya LGT Holdings ambayo inajiendesha
kwa faida kubwa tofauti na familia nyingine za kifalme ambazo zina utajiri
unaotokana kwa kiasi kubwa na kodi za wananchi wao.
|
No comments:
Post a Comment