RATIBA YA SOKA:-Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia raundi ya 12 Jumamosi Januari 24 na 25,2015 kwa mechi Saba….Soma hapa Timu yako itacheza na Nani.??. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 23, 2015

RATIBA YA SOKA:-Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia raundi ya 12 Jumamosi Januari 24 na 25,2015 kwa mechi Saba….Soma hapa Timu yako itacheza na Nani.??.

Ligi kuu ya soka Tanzania bara 2014/2015 itaendelea kesho Januari 24,2015,Jumamosi huku mechi kadhaa zikichezwa ikiwemo ile kati ya Bingwa mtetezi na wawakilishi wa nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Azam FC na Simba Sports Club ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic.

Azam FC inaongoza ligi ikiwa na pointi 20 na baada ya mechi yao na Simba SC itaenda Jamhuri ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kucheza mechi za majaribio kwa ajili ya mechi yao na vigogo wa Sudan, El-Merreikh katika mechi ya kwanza klabu bingwa Afrika itakayochezwa Dar es Salaam kati kati ya mwezi ujao.

Mabingwa wa zamani wa Tanzania na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga SC, ikiwa ya nne katika msimamo na alama (points) 15, watacheza na Polisi Morogoro wakati Mtibwa Sugar, ikiwa ya pili na alama 17, watacheza na Ruvu Shooting.

Kesho (Januari 24 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Morogoro na Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mechi za Jumapili Januari 25,mwaka huu ni kati ya Azam FC na Simba SC (Uwanja wa Taifa).

 Kagera Sugar na Ndanda FC (Uwanja wa CCM Kirumba).

Stand United na Coastal Union (Uwanja wa Kambarage).

Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine).

Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Mabatini).

na JKT Ruvu na Mgambo Shooting (Uwanja wa Azam Complex).

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad