MALEZI YETU:-Watazame Katika Picha Watoto waliosafiri ndani ya Buti ya Basi kutoka Kabanga wilayani Ngara hadi Buziku kisha Kugunduliwana na Kurudishwa......Eti wanaenda Mwanza.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 12, 2015

MALEZI YETU:-Watazame Katika Picha Watoto waliosafiri ndani ya Buti ya Basi kutoka Kabanga wilayani Ngara hadi Buziku kisha Kugunduliwana na Kurudishwa......Eti wanaenda Mwanza..

Kwa mujibu wa Abiria waliokuwa wanasafiri na Basi la Kampuni ya Nyehunge namba #2 utoka wilayani NGARA mkoani Kagera kwenda Jijini MWANZA Januari 11,2015,wanasema Watoto hao wawili wa Kike na Kiume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 8 hadi 9 walikutwa ndani ya Buti la mizigo la Basi hilo katika Standi ya Buziku wakati Basi likipakia abiria ndipo Kondakta wake alipotaka kuweka mizigo katika Buti kuwaona.

Watoto hao  wawili walitambuliwa na Mama mmoja ambaye alikuwa akisafiri na basi hilola Nyehunge,kuwa ni Watoto wa familia moja inayoishi Mjini Kabanga ,wilayani NGARA na ndipo Wafanyakazi wa basi hilo walipofanya jitihada za Kuwapakia katika Basi lao jingine lililokuwa likitoka MWANZA kuja NGARA ili kuwarudisha KABANGA kwa wazazi wao.




Inasemekana watoto hao Waliingia ndani ya Buti za Basi hilo bila kugundulika wakati Likipakia Mizigo katika stendi ya KABANGA na walidai walikuwa wanataka kwenda MWANZA huku huko wakiwa hawana ndugu.

Mwana wa Makonda Blog inatoa wito kwa Wazazi na Walezi kuhakikisha wanakuwa makini kwa Watoto wao hasa kuwapa malezi mema na matunzo stahiki ili kuwajenga katika msingi wa kuishi maisha ya kuthaminika/upendo kutoka kwa Wazazi wao.

Picha Na:-Mwanawamakonda WhatsApp +255789925630.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad