AJALI :-Basi lateketea na kuua Zaidi ya Watu 50 Pakistani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 11, 2015

AJALI :-Basi lateketea na kuua Zaidi ya Watu 50 Pakistani.

Pichani juu na chini ni Taswira kutoka ndani ya basi hilo la abiria likiwa limeteketea baada ya ajali.

Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa Hospitali ya Jinnah, Karachi.

WATU zaidi ya 50 wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana na lori la mafuta kisha magari yote kuteketea kwa moto jirani na Mji wa Karachi nchini Pakistan.

Imeelezwa kuwa lori la mafuta lilikuwa katika spidi kali lilipogongana uso kwa uso na basi hilo.

Basi lilikuwa limebeba watu zaidi ya 60 na lilikuwa likielekea kwenye Mji wa Shikarpur kutokea Karachi.

Dk. Seemi Jamali, mkuu wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Jinnah mjini Karachi amesema kuwa wamepokea miili ya watu 57 huku akiongeza kuwa idadi inaweza kuongezeka.

Chanzo: BBC
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad