Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw.John Mongella
akisalimiana na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Bw.Musoni Protais kabla ya
uzinduzi wa daraja la Rusumo,mwingine ni Rais wa JICA Dkt Tanaka.Picha/Habari
Na:-Shaban Ndyamukama.
Shirika la
Ushirikiano na Misaada ya Kimataifa la Japan (JICA) limekabidhi Mradi wa
Ujenzi wa daraja la Kimataifa la Rusumo
na kituo cha utoaji wa huduma za pamoja kwa nchi za Tanzania na Rwanda.
Miradi ya
vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja imejengwa kwa nchi zote mbili ambapo
Makabidhiano yameshuhudiwa na Rais wa (JICA Dkt. Akihiko Tanaka katika sherehe fupi
iliyofanyika upande wa Rwanda katika Wilaya ya Kirehe Januari 10,2015.
Imeelezwa
kuwa mradi wa kujenga vituo hivyo vya forodha kwa nchi hizo mbili umegharimu
kiasi cha dola 32 milioni za kimarekani na ujenzi wa miundombinu ya vituo hivyo
umefikia kiwango cha kuanza kutumika.
|
No comments:
Post a Comment