UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015:- Arsenal waichapa Dortmund 2-0 huku Meneja Arsène Wenger akifurahia kufuzu kwa mara ya 15 Mfululizo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 27, 2014

UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015:- Arsenal waichapa Dortmund 2-0 huku Meneja Arsène Wenger akifurahia kufuzu kwa mara ya 15 Mfululizo.


Furaha ya Meneja wa Washika bunduki wa Jiji la London, Arsène Wenger kufuzu kwa mara ya 15 mfululizo kutinga Raundi ya Mtoano kutoka kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya Jana November 26,2014,kuichapa Borussia Dortmund iliingia dosari kufuatia kuumia kwa Nahodha wake Mikel Arteta.

 Jana Arsenal waliichapa Dortmund 2-0 wakiwa kwao Emirates kwa Bao za Yaya Sanogo na Alexis Sanchez na kusonga pamoja na Dortmund toka Kundi D huku wakiwa na Mechi moja mkononi.

Lakini ushindi huo uliingia dosari baada ya Arteta kulazimika kutoka Uwanjani baada kuumia Musuli za Mguuni na kufanya idadi ya majeruhi wa Arsenal kutoka Timu ya kwanza kufikia 10.

Pamoja na Arteta, majeruhi mwingine toka Mechi hiyo na Dortmund ni Yaya Sanogo alieumia Musuli za Pajani mwishoni mwa Mechi.


Jumamosi, walipofungwa na Man United 2-1 huko Emirates, Arsenal walimpoteza Jack Wilshere alipoumia Enka na Leo anamwona Mtaalam kujua kama anahitaji operesheni au la lakini inakadiriwa atakuwa nje kwa Miezi Mitatu.

Majeruhi wengine wa Arsenal ni Mesut Özil, Theo Walcott, Danny Welbeck, Mathieu Debuchy, Abou Diaby, Wojciech Szczesny na David Ospina.

Wenger ameeleza: “Hali hii ya majeruhi ni tatizo kwani tuna Mechi nyingi na Leo tumepoteza wawili.”

Kuhusu kufuzu kwao kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Wenger alisema safari hii anaomba wawe na bahati baada ya kupata Droo ya Mechi ngumu mara 4 zilizopita na kutolewa nje kwenye Raundi hiyo.


Kwa Miaka Minne iliyopita Arsenal wamekuwa wakiishia Raundi hii baada ya kupangwa na kubwagwa nje na Barcelona, AC Milan na mara mbili na Bayern Munich.

Huku akitania, Wenger alisema: “Kwanza tumtumie Mtu mwingine kwenye Droo ya Raundi ya Mtoano. Sababu ukiangalia rekodi yetu, mara zote tunapangwa na Timu ambazo huzitaki. 

Ulaya Timu zote ziko juu lakini zipo 3 au 4 ambazo hutaki kukutana nazo.”


MATOKEO UEFA 2014/2015 -Jumatano Novemba 26,2014.

Zenit St. Petersburg 1 Benfica 0     

Arsenal 2 BV Borussia Dortmund 0   

Atletico de Madrid 4 Olympiacos 0      
  
Bayer 04 Leverkusen 0 AS Monaco 1   

FC Basel 0 Real Madrid 1   
   
Malmö FF 0 Juventus 2    
   
RSC Anderlecht 2 Galatasaray Spor Kulübü 0  
   
Ludogorets Razgrad 2 Liverpool 2

MSIMAMO UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015.


KUNDI A
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Atletico Madrid
5
4
0
1
14
3
11
12
Juventus
5
3
0
2
7
4
3
9
Olympiacos
5
2
0
3
6
11
-5
6
Malmo
5
1
0
4
2
11
-9
3
KUNDI B
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Real Madrid CF
5
5
0
0
12
2
10
15
FC Basel 1893
5
2
0
3
6
7
-1
6
PFC Ludogorets
5
1
1
3
5
10
-5
4
Liverpool FC
5
1
1
3
4
8
-4
4
KUNDI C
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Bayer Leverkusen
5
3
0
2
7
4
3
9
AS Monaco
5
2
2
1
2
1
1
8
FC Zenit St Petersburg
5
2
1
2
4
4
0
7
Benfica
5
1
1
3
2
6
-4
4
KUNDI D
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Borussia Dortmund
5
4
0
1
13
3
10
12
Arsenal FC
5
3
1
1
11
7
4
10
RSC Anderlecht
5
1
2
2
7
9
-2
5
Galatasaray AŞ                  
5
0
1
4
3
15
-12
 1


TIMU ZIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO.

-Real Madrid CF

-FC Barcelona

-Paris Saint-Germain

-Borussia Dortmund

-FC Bayern Munich 

-FC Porto 

-Shakhtar Donetsk

-Chelsea

-Arsenal

-Atletico Madrid

-Bayer Leverkusen

**BADO TIMU 7
**Timu zinazomaliza Nafasi ya 3 zinapelekwa EUROPA LIGI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad