MTIKISIKO WA TANO NCHINI TANZANIA:-Ni kuhusu Kamati ya hesabu za serikali PAC yaanika madudu ya ESCROW na mapendekezo ya kuchukuliwa Wahusika wake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 27, 2014

MTIKISIKO WA TANO NCHINI TANZANIA:-Ni kuhusu Kamati ya hesabu za serikali PAC yaanika madudu ya ESCROW na mapendekezo ya kuchukuliwa Wahusika wake.

Ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) imependekeza kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, naibu wake na katibu mkuu wa wizara hiyo wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

 Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kutunza fedha za gharama za uwekezaji (capacity charge) baada ya kuibuka mzozo wa kimkataba baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni binafsi ya IPTL ambayo iliingia mkataba wa kufua umeme na kuliuzia nishati hiyo shirika hilo la umma.

Ripoti hiyo ilisomwa jana November 26, 2014, bungeni kwa kupokezana kati ya Mwenyekiti wa PAC,Bw. Zitto Kabwe na Makamu mwenyekiti, Bw.Deo Filikunjombe baada ya majadiliano marefu kwenye vikao vya ndani vya CCM na Kamati ya Uongozi wa Bunge na jitihada kubwa za kutaka isisomwe na kujadiliwa.

Ripoti hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa uchotaji wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Pinda ametiwa hatiani na kamati hiyo kutokana na kujua kuwapo kwa ufisadi huo na kauli zake kuwa fedha hizo hazikuwa mali ya umma, wakati Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo, wakati Waziri Sospeter Muhongo hakuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa sakata hilo, huku naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya Bunge.

Kamati pia imependekeza uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi utenguliwe kutokana na kuingia makubaliano ya kutoa fedha bila ya kujiridhisha kikamilifu kuhusu uamuzi wa hukumu ya mahakama ya Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Kiuwekezaji (ICSID).

Iwapo mjadala huo, unaotazamiwa kuendelea leo November 27, 2014, utaafiki hatua hizo zichukuliwe, Rais atalazimika kuunda Serikali upya kwa mara ya pili tangu alipofanya hivyo mwaka 2008 wakati wa sakata la Richmond, ambalo lilihusu umeme. 

Pia atakuwa akifanya mabadiliko ya mawaziri kwa mara ya tano kutokana na wasaidizi hao kujikuta kwenye kashfa.

“…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.

Kwa upande wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; -

Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi Bil. 1.6.

Mheshimiwa Anna Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, shilingi Bil. 1.6.

Mheshimiwa William Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, shilingi milioni 40.4.

Ndugu Daniel Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4.

Ndugu Paul Kimiti, ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na ndugu Enos Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCo aliingiziwa shilingi milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad