LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Chelsea, Manchester City zang’ara Ligi Kuu November 22,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 23, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Chelsea, Manchester City zang’ara Ligi Kuu November 22,2014.


Kocha Louis Van Gaal alipata ushindi wake wa kwanza ugenini kama meneja wa Manchester United baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi Arsenal na hivyo  kupanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya soka Ungereza EPL hapo Jana November 22, 2014.
Baada ya kuonyesha mchezo mzuri kwa kipindi kirefu,Kiaran Gibbs alijifunga kufuatia krosi nzuri katika lango la Arsenal iliopigwa na Antonia Valencia kabla ya Wayne Rooney kukamilisha mambo na kuwa 2-0.

Olivier Giroud ambaye aliingia katika kipindi cha pili alifunga bao moja ambalo halikuweza kuimarisha matumani ya Arsenal.

Huku Van Gaal akisheherekea ushindi huo ,matokeo hayo yanaiwacha Arsenal ikiwa na alama 17 kutoka mechi 12 walizocheza ikiwa ni alama kidogo kwa kipindi cha miaka 32 katika ligi ya Uingereza.

Katika matokeo mengi,Chelsea imeendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza  ikiwa na pointi 32 bila mpinzani baada ya kuilaza West Brom kwa mabao 2-0.

Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard, kipindi cha kwanza yaliiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi dhidi ya West Brom iliyocheza muda mrefu na wachezaji 10 baada ya Claudio Yacob kutolewa kwa kadi nyekundu.

Nao, Manchester City waliilaza Swansea kwa mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Etihad.

Swansea walitangulia kufunga bao kupitia kwa Wilfried Bony kabla ya Steven Jovtric kusawazisha na Yaya Toure kumaliza kazi, kipindi cha pili.

Kwingineko matokeo yalikuwa:-Everton 2-1 West Ham, Newcastle 1-0 QPR, Stoke 1-2 Burnley, Leicester 0-0 Sunderland.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad