HAPATOSHI:-Ni kuhusu Wabunge wa upinzani wadai ripoti imechakachuliwa.'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 23, 2014

HAPATOSHI:-Ni kuhusu Wabunge wa upinzani wadai ripoti imechakachuliwa.''

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai......Picha ya maktaba yetu.

  Hali ni tete. Ndiyo neno ambalo unaweza kulizungumza kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mji wa Dodoma tangu juzi November 21,2014,umejaa pilikapilika zikiambatana na mikutano iliyokuwa ikijadili kashfa hiyo.

Kamati ya Uongozi wa Bunge, Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa CCM, Baraza la Mawaziri, kwa nyakati tofauti walikaa kujadili ripoti ya escrow ambayo inatarajiwa kujadiliwa na Bunge Jumatano na Alhamisi wiki hii.

Leo kikao cha wabunge wa CCM kinatarajiwa kufanyika kujadili suala hilo. 

Wabunge walionekana kila kona ya Viwanja vya Bunge jana wakijadiliana katika vikundi kuhusu sakata la escrow, huku wengine wakitaka hata miswada yote iliyobaki isijadiliwe ili kutoa nafasi kuichambua kwa kina kashfa hiyo.

Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo.

Wabunge wa CCM wamegawanyika katika makundi matatu; linaloshinikiza waliohusika na wizi huo wajiuzulu, kundi la watu wasiokuwa na msimamo na kundi linalotaka ripoti isijadiliwe bungeni.

Kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja iliyokuwa imepangwa awali.
Kamati ya Uongozi CCM.

Katika kikao cha Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa CCM, wabunge wawili akiwemo Naibu Spika, Job Ndugai walipewa kibano kuhusiana na matamshi yao kuhusu sakata hilo.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa waliokumbana na kibano hicho ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, ambao waliambiwa kwamba matamshi yao wakati wakichangia yalilenga kukifanya chama hicho kuonekana kuwa ni cha wezi.

“Ndugai yeye walimbana kwa nini aliruhusu mjadala huo bungeni,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Aidha, baadhi ya wabunge wana hofu kuwa mjadala huo huenda usiende bungeni.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad