Waziri wa Afrika mashariki Samwel Sitta aanza ziara mkoani Kagera lengo kuhamasisha mapokeo kwa wananchi juu ya jumuiya hiyo ya EAC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 28, 2012

Waziri wa Afrika mashariki Samwel Sitta aanza ziara mkoani Kagera lengo kuhamasisha mapokeo kwa wananchi juu ya jumuiya hiyo ya EAC.


Waziri wa Afrika mashariki Samwel Sitta ameanza ziara ya kuzungukia sehemu za mipaka mkoani Kagera na kukagua hali ya maendeleo na mapokeo ya wananchi juu ya  jumuiya hiyo ya EAC.


Mkoa wa Kagera unapatikana kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania ambapo  Makao makuu ya mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam.

Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa kaskazini, Rwanda na Burundi ,kwa upande wa magharibi mkoa wa Kigoma, Mwanza kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa upande wa mashariki.


 Vile vile mkoa wa Kagera uko kusini mwa ikweta kati ya 1 “00” na 2”45” latitudi. Kwa Iongitudo uko katika nyuzi 30”25” na 32”40” Mashariki mwa ‘greenwich'.


Mkoa wa Kagera ulijulikana kama “Ziwa Magharibi” jina hili lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda.



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe akitoa taarifa kwa Waziri Swamwel Sitta Waziri wa Afrika Masharik.


Mkoa ulipata jina hili kutokana na mto Kagera ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria.


Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168 kati ya hizo kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu za kilomita 10,655 ni eneo la maji. 

Ukiacha mbali wilaya za Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad