Nbii wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza
Kipera jijini Dar Es Salaam, Yaspi Bendera.
NABII wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi
Bendera amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono
anayoyaona wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano
linakupa mkanda kamili.
Akizungumza
wakati wa ibada kanisani kwake na baadaye na waandishi wetu Novemba 16 mwaka
huu, Nabii Yaspi alisema kuna mgongano mkubwa miongoni mwa watu wanaotajwa
kugombea urais, ili kumrithi rais Jakaya Kikwete ambaye alimwelezea kama
kiongozi anayemuona kiroho kila mara.
“Nilimuona
katika maono yangu kama mtu aliye kwenye majaribu makubwa kiroho, nikaandaa
maombi hapa kanisani na tukamuombea kwa muda wa nusu saa na tunashukuru Mungu
hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini
Marekani.
Bado namuona akiwa na maumivu kuanzia sehemu za kiuno, uti wa mgongo
na shingoni mwake.
Mhe. Edward Lowasa.
“Hivi sasa
ninapomuombea atasikia moto unawaka na kupita kwenye sehemu hizo na kuwa mzima
kabisa.
Tunamuombea baraka na uzima rais ili aweze kukabidhi madaraka vizuri
kwa rais ajae,”alisema Nabii huyo na kuongeza kuwa alilazimika kumuombea rais
ili asipatwe na madhara kwani kama hali hiyo ingetokea, kungekuwa na vurugu
kubwa kuelekea wakati wa Uchaguzi mkuu.
Waandishi
wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia Nabii Yaspi akiwa ameshika picha ya
Rais na waumini wake wakizama katika maombi kwa ajili ya Rais Kikwete huku na
walipomaliza alisema tatizo lake limemalizika.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Kana kwamba
haitoshi, Nabii huyo alisema baadhi ya wagombea urais wanapita kwa waganga wa
kienyeji lakini akasema hawatafanikiwa kwa kuwa yeye anaomba Rais ajaye atoke
kwa Mungu kwa kuwa yeye atakuwa nyuma ya mgombea huyo bila kujali chama
anachotoka.
Nje ya
ukumbi wa kanisa, Nabii huyo alizungumza na waandishi wetu ambao walimuuliza
kuhusu jinsi anavyoona kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
Vipi kuhusu utafiti wa
Twaweza
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Kuhusu
utafiti uliotolewa hivi karibuni kuhusiana na uchaguzi mkuu kama
ulivyowasilishwa na taasisi ya Twaweza, ambao umewagawa wananchi, Nabii huyo
alisema anaunga mkono kwani umefanywa kwa usahihi kwa vile ndivyo hata yeye
anavyoona.
“Utafiti
umefanywa vizuri na nadhani kila kitu kipo kama kilivyoainishwa, lakini kama walivyosema
wenyewe kwenye ripoti yao, upepo unaweza kubadilika wakati wowote maana miujiza
ya Mungu huja bila kutarajiwa,” alisema.Nani atashinda Urais?
Wazari wa mambo ya nje Benard Membe.
“Hivi
unauliza swali kama hilo kweli wakati huu? Ripoti iliyotolewa imemaliza kila
kitu na majibu yako wazi kabisa,” alisema nabii huyo bila kutoa ufafanuzi
zaidi.
Utafiti
uliotolewa na taasisi hiyo ya Twaweza uliotolewa hivi karibuni, ulisema kuwa
endapo Uchaguzi mkuu wan chi ungefanyika hivi sasa, Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa angeibuka mshindi, huku akifuatiwa kwa karibu na Waziri Mkuu wa
sasa, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akiibuka
katika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment