Baada
ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita,
iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’
ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na
kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo
sasa ameibuliwa afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Kwa
mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari
wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme,
inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa
katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye,
ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa
kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura,
umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa
katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari
zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil
Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira
ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana kwamba, Linga ndiye
aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa
walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba
baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera
yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni
dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali
isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga
kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze
kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
kilidai chanzo hicho.
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa
kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama
wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua
na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo
ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.
Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo
alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili
kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao
na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha,
lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho,
kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru
Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo
walichokifanya ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga
alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi
kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo
tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako
alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa
kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye
kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao
mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na
kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari
vilivyoamua kuripoti.
kilisema chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika
hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa
akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa
moja kama kweli ni yeye (angalia picha hapo juu).
Kwa mujibu wa maoni lukuki katika
mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa
aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba
hayo.
ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi,
meza yetu ya habari imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry
Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa
kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi
Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema
walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu
Mwaibambe.
Habari Na:-Malunde Blog.
Karibu
kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana
/Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment