KUUNGUA KWA LORI LA MAFUTA:-Hii ndiyo Taswira ya Majeruhi wa Moto wa petrol waliolazwa Hospitali ya Muhimbili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 16, 2014

KUUNGUA KWA LORI LA MAFUTA:-Hii ndiyo Taswira ya Majeruhi wa Moto wa petrol waliolazwa Hospitali ya Muhimbili.


Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa  wodini.

Majeruhi 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.

Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.

Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni  Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).

Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.

(Picha/Habari na Haruni Sanchawa/GPL)




Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad