Tazama Gari lililoshambuliwa na waasi wakati Wanajeshi wa Tanzania wakisindikiza na kutoa ulinzi kwa waangalizi wa amani Darfur. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 30, 2013

Tazama Gari lililoshambuliwa na waasi wakati Wanajeshi wa Tanzania wakisindikiza na kutoa ulinzi kwa waangalizi wa amani Darfur.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi hapa nchini Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange amesema wanajeshi hao walishambuliwa na waasi wakati wakisindikiza na kutoa ulinzi kwa waangalizi wa amani na washauri wa polisi na kwamba walipopunguza mwendo kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua umbali wa kilomita 25 kutoka Darfur ndipo waliposhambuliwa.






Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete akiongozana na viongozi mbalimbali waandamizi katika serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na watu maarufu  katika kuiaga miili saba ya wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania waliouwawa nchini Sudan Jumamosi ya July 13 mwaka huu.

Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Dr Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo akionekana dhahiri shairi mwenye majonzi  ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kuwaongoza mamia ya waombolezaji kuiaga miili ya wanajeshi hao waliouwawa na kikundi cha waasi nchini Sudan katika jimbo la Darfur amesema taarifa za tukio hilo limemuhuzunisha,kumsikitisha na kumkasirisha na kushauri kuwa wakati umefika wa kuutazama upya mfumo mzima wa kulinda amani Darfur hasa kuhusu kiwango cha uwezo wa wanajeshi kujilinda kutokana na ukweli kuwa tayari walinda amani 41 kutoka mataifa mbalimbali wameuwawa na wengine 55 kujeruhiwa.


Aidha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Mh Shamsi Vuai Nahodha amekiita kitendo cha wanajeshi hao wakulinda amani kuuwawa ni dhahiri tendo ovu ambao ni mkakati maalum wa waasi kutaka kuhakikisha mpango wa umoja wa mataifa katika kuleta amani katika nchi zenye mifarakano hazifanikiwi huku aliyekuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr Asha Rose Migiro akisema tukio hilo lisiwakatishe tamaa katika kupigania amani ya watu wengine katika nchi zenye mifarakano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad