Tazama Matukio ya Zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 30, 2013

Tazama Matukio ya Zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge.


Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Deogratius Ntukamazina  akikata Utepe wakati wa Ufunguzi wa  Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) katika kituo cha Walimu (TRC) Mjini Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge.

Muonekano wa vitambu (Elfu 2018) Vya aina mbalimbali katika  Maktaba ya Wilaya ya Ngara vyenye thamani ya shilingi milioni 36 na Laki 9 na 67,000  ambapo katika  Maktaba ya Tarafa ya Rulenge Jumla ya Vitabu(Elfu 1222) Vya aina mbalimbali vikipatikana na Vinathamani ya Shilingi Milioni 17,Laki 3 na 68,000.
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria ufunguzi  wa maktaba hizo mbili  ambapo Jamii imetakiwa kujitokeza kutumia huduma za Maktaba hizo  kwa kujisomea Vitabu mbalimbali ili kujiongezea Maarifa.

Afisa Michezo na Utamaduni wilaya ya Ngara Bw.Said Salumu akiwa ni mshereheshaji mkuu katika  zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo jana(Julai 29,2013).

Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la NgaraBw.Deogratius Ntukamazina (Mkewe kushoto yake) , Mkurugenzi wa Bodi ya Maktaba nchini Bw Ally Mcharazo, Mhadhiri wa chuo kikuu cha London na Afisa Elimu wilaya ya Ngara Bw.Saimon Mumbee wakati wa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013).

Afisa Elimu wilaya ya Ngara Bw.Saimon Mumbee akimkaribisha Mrs. Ntukamazina Mke wa Mbunge wa Jimbo la Ngara  wakati wa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) Mjini Ngara.

Wadau waliojitokeza kushuhudia  zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) wakitazama vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika Maktaba hizo.

Mwanafunzi akisimulia hadithi kutoka moja ya vitabu alivyosoma Maktaba mbele ya wenzao wakati wa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) Mjini Ngara.

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Ngara ,Mrs. Ntukamazina akisalimiana na Mkurugenzi wa Bodi ya Maktaba nchini Bw Ally Mcharazo wakati wa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) Mjini Ngara.

Baadhi ya Walimu wa Kata ya Rulenge wakati wa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara na Maktaba ya Tarafa ya Rulenge hapo Jana(Julai 29,2013) katika Kituo cha Walimu (TRC) Mjini Rulenge.

Mke wa Mbunge wa Jimbo la Ngara kushoto(Mrs. Ntukamazina) akiwa na mke wa mkurugenzi wa bodi ya maktaba Tanzania(Mrs. Mcharazo).

Mkaguzi mkuu wa shule wilayani Ngara Wilfred Majige na Mhadhiri wa chuo kikuu cha London ambaye ni  mmoja wa wafadhili wa vitabu Vyenye Jumla ya  thamani ya Shilingi milioni 54,23,5000  vinavyopatikana katika maktaba ya wilaya ya Ngara na Maktaba ya Taarafa ya Rulenge wakikagua vitabu katika Maktaba ya Wilaya katika kituo cha  TRC Mjini Ngara.

Muonekano wa vitambu (Elfu 2018) Vya aina mbalimbali katika  Maktaba ya Wilaya ya Ngara vyenye thamani ya shilingi milioni 36 na Laki 9 na 67,000  ambapo katika  Maktaba ya Tarafa ya Rulenge Jumla ya Vitabu(Elfu 1222) Vya aina mbalimbali vikipatikana na Vinathamani ya Shilingi Milioni 17,Laki 3 na 68,000.

Toka Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Deogratius Ntukamazina  akiwa na Ofisa Elimu wilaya ya Ngara Bw.Simon Mumbee na Mkaguzi mkuu wa shule wilayani Ngara Bw.Wilfred Majige mara baada ya kumalizika kwa zoezi la Ufunguzi wa Maktaba ya Wilaya ya Ngara hapo Jana(Julai 29,2013) katika kituo cha Walimu (TRC) Mjini Ngara wakiwa katika picha ya pamoja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad