Lady Jaydee
(kulia) akiwa na Prof. Jay (kushoto) pamoja na Gadna (kwa nyuma) wakiwa
wanatoka mahakamani jana(Julai 30,2013).
|
Lady Jayde
akiwa anatoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
|
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kinondoni, Jana(Julai 30,2013) imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi
kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa
Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya
madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya
kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee
kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu
kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na
kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya
madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa
Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa mujibu
wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye
ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.
No comments:
Post a Comment