Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Sudi achaguliwa kuwa mwenyekiti Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 24, 2012

Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Sudi achaguliwa kuwa mwenyekiti Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Ngara mkoani Kagera.


Bw Said Sudi.
Jumuiya  ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Ngara mkoani Kagera imemchagua Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Sudi kuwa mwenyekiti mpya atakayeiongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ngara ,msimamizi wake Bw Wilbad Bambara amesema Bw.Soud amepata kura 241 kati ya kura 259 zilizopigwa. 


 
Bw Bambara amesema mgombea mwingine Bw Allan Mnanga amepata kura  14 .


Aidha Bw Bambara amewataja wajumbe 3 wa mkutano mkuu wa taifa wa jumuiya ya wazazi waliochaguliwa kuwa ni Bw Mungele Kafiriti, Bi Elida   Mhimbiza na Philimon Mpanju.


Akizungumza mara baada ya Kuchaguliwa Bw.Sudi amewataka wana Jumuiya hiyo kushimamana na kushirikiana kuiweka na kuijenga jumuiya ya wazazi wilaya ya Ngara ikae katika madhumuni ya kuanzishwa kwake.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad