
Na Mohammed
Mhina, Jeshi la Polisi Zanzibar.
Kampuni ya
Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya
na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.
Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini
Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake na kwamba meli
hiyo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu
za mamlaka mbalimbali.
![]() |
Sehemu ya
Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
|
![]() | ||
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kupumzikiazikia wasafiri. |

Bw. Hussein
amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo
maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo
magari.
Amesema meli
hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4
kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
Amesema
pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli
nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
![]() |
Mzee Said
Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya
kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
(Picha na
Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
|
Kwa upande
wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo
lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na
kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.
Bwana Rajabu
Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna
haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri
kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.
No comments:
Post a Comment