Basi la Adventure
likiwa na mizigo ndani ya buti ikiteketea
na moto.
|
Watu 63
wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mwanza
kwenda mkoani Kigoma, kuwaka moto.
Tukio hilo
limetokea leo majira ya saa nne na nusu asubuhi katika kijiji cha Nyantakala
wilayani Biharamuro, Mkoani Kagera, likihusisha gari aina ya Scania lenye namba
T 928 AVP, mali ya Kampuni ya Adventure ya jijini Mwanza.
Juu ni
mwonekano wa basi la adventure baada ya kuungua huku picha ya chini baadhi ya
wananchi wakipakua badhi ya mizigo ambayo imesalia ndani ya basi hilo.
|
Kwa mujibu
wa taarifa zilizopatikana kutoka wilayani Biharamuro, watu 8 kati yao
wamejeruhiwa kwa moto na wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe
mkoani Geita, kwa matibabu zaidi.
Chanzo ajali
hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika betri ya Gari hilo ambapo hadi sasa gharama halisi ya mali za abiria
zilizoteketea kwa moto bado haijajulikana.
No comments:
Post a Comment