 |
Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu
umeongezeka kwa asilimia saba.
Jumla ya
watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya
mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio
wamefaulu ambapo wasichana ni 143,728
sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.
Akitangaza
matokeo hayo Jana Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016
watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.
Amesema
matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka
huu.
"Watahiniwa
77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani
watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.
Dk Msonde
amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja
akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.
|
BOFYA HAPA CHINI
KUYATAZAMA MATOKEO YOTE.
Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt)
2017
No comments:
Post a Comment