Wanawake Wajawazito wametakiwa kufika mapema katika Vituo vya Afya,
Zahanati na Hospitali hasa wanapokaribia kujifungua ili
kuepuka kujifungulia njiani.
Hayo yamesemwa na muuguzi wa kituo cha afya Bunazi Bi Blandina Bahati muda
mfupi baada ya kumpokea mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha
Ibanga kata ya Nsunga wilayani Missenyi mkoani Kagera
ambaye amejifungulia njiani wakati akitembea kwa mguu
kuelekea kituoni hapo.
Bi Lethicia Didas akiongea na Radio Kwizera mara baada ya
kufika kituoni hapo kupatiwa huduma amesema alipata
uchungu kabla hajafika kituoni ndipo akalazimika kujifungulia kwenye shamba la miwa bila
kuwa na msaada kutoka kwa wataalam tofauti na ndugu yake aliyekuwa
anamsindikiza.
Nae Bi Peace Elnest aliemsindika mama
huyo amesema chanzo cha kujifungulia njiani ni ukosefu wa
fedha ya nauli ambapo kutoka nyumbani hadi
kufika kituo cha afya Bunazi ni umbali wa kilometa 15 na
usafiri wa pikipiki unagharimu kiasi cha shilingi elfu tano.
|
No comments:
Post a Comment