Mwanafunzi
wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Tumaini Manispaa ya Bukoba Akiendelea Kufanya
Mtihani wa Somo la Kiingereza.
|
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Gaguti Akiangalia Ratiba ya Mtihani Wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Mafumbo Manispaa ya Bukoba. |
Wanafunzi wa
Darasa la Saba Wakiendelea Mtuhani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi .
|
Wanafunzi wa
Darasa la Saba Wakiendelea Mtuhani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi.
|
Mkuu wa Mkoa
Kagera Mhe. Gaguti Akiongea na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tumaini
Augustina Daniel Kujua Kama Kuna Changamoto Yoyote Iliyojitokeza Katika Shule
Yake.
|
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti
Mara Baada ya Kukagua na Kujiridhisha na Maendeleo ya Namna Mtihani
unavyfanyika Anasaini Kitabu cha Wageni Shule ya Msingi Mafumbo.
Na: Sylvester Raphael.
Mkoa wa
Kagera ukiwa mkoa mmoja wapo kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo wanafunzi wake wa Darasa la Saba Wavulana 22,129 na Wasichana 25,099 jumla
47,228 wanafanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi maandalizi kuanzia
kuwaandaa wanafunzi, Mapokezi ya Mtihani hadi siku ya kwanza ya kufanya mtihani
Septemba 5, 2018 na mtihani huo kufanyika hali ni shwari na mtihani umefanyika
kama ilivyopangwa.
Kikiwa
kipaumbele chake cha kwanza kuhakikisha Mkoa wa Kagera unaendelea kufanya
vizuri na kushika nafasi za juu kabisa Kitaifa tangu kuripoti kwake Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alipata nafasi ya kutembelea
baadhi ya shule katika Manispaa ya Bukoba ili kuona mitihani hiyo kama
inaendelea kufanyika kama Mkoa ulivyojiandaa na kujipanga ifanyike.
Baada ya
kutembelea shule za Msingi kadhaa katika Manispaa ya Bukoba ikiwemo Shule za
Msingi Tumaini na Mafumbo na kuongea na wasimamizi wakuu wa vituo na Walimu
Wakuu wa Shule hizo Mkuu wa Mkoa Gaguti aliridhika na maendeleo ya wanafunzi
wanavyofanya mtihani pia na usimamizi unavyoendelea kuimarishwa kuhakikisha
hakuna udanganyifu wowote.
“Hadi sasa
hakuna changamooto yoyote katika Mkoa wetu wa Kagera ambayo nimeipokea kuhusu
kufanyika kwa Mitihani ya Darasa la Saba, aidha, na mimi mwenyewe nimepita
katika shule kadhaa kuona namna zoezi hili linavyoendelea, naona wahusika wote pamoja
na wanafunzi wanaendelea na majukumu yao bila wasiwasi.” Alifafanua Mkuu wa
Mkoa Gaguti.
Pia Mkuu wa
Mkoa Gaguti alitoa rai kwa watendaji wote waliokabidhiwa jukumu la kusimamia Mitihani
ya Darasa la Saba kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa kusimamia Mitihani hiyo
kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hadi mitihani itakapokamilika na
kukabidhiwa mahali panapohusika bila kujihusisha na vitendo vyovyote vya hujuma
vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Ufaulu
wa Mitihani ya Darasa la Saba Mkoa wa Kagera: Kwa ujumla Mkoa wa Kagera ni
miongoni mwa Mikoa inayofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la
saba.
Mwaka 2017 ulishika nafasi 3 kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara ikilinganishwa na nafasi ya 5 mwaka 2016 kati ya Mikoa 26 ya
Tanzania Bara pia ikilinganishwa na nafasi ya 7 mwaka 2015 kati
ya Mikoa 25 na nafasi ya 8 mwaka 2014 kati ya Mikoa 25.
Mkuu wa Mkoa
Gaguti amewatakia heri na ufaulu mzuri wanafunzi wote wanaofanya Mtihani wa
Darasa la Saba Mkoani Kagera na kusema kuwa imani yake mwaka huu Mkoa wa Kagera
utongoza Kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa.
Jumla ya Shule 953 Katika Mkoa wa Kagera 890
zikiwa za Serikali na 63 Binafsi zenye watahiniwa jumla 47,228 zinafanya
Mtihani wa Darasa la Saba.
|
No comments:
Post a Comment