![]() |
“Ninayo taarifa kuwa Kagera tunavyo viwanda vikubwa tisa
lakini vinazalisha chini ya kiwango kutokana na kukosa malighafi zinazotakiwa
kuzalishwa kutokana na kutopatikana kwa wingi. Sasa umefika wakati wakulima
kuachana na kilimo cha mazoea cha kulima ekari kumi na kupata gunia 10 bali
mkulima alime ekari moja avune gunia 20 za mazao, pia kuachana na ufugaji wa
kufuga ng’ombe kumi na kupata lita 10 za maziwa bali mfugaji afuge ng’ombe
mmoja apate lita 20 za maziwa.” Alifafanua Gaguti.
Mkuu huyo wa
Mkoa wa Kagera, alifafanua zaidi kuwa mkoa wa Kagera unayo fursa kubwa zaidi ya
kilimo kwani hali ya hewa na ardhi yake inaruhusu kilimo cha zao lolote kwa
hiyo wananchi wanatakiwa kuitumia fursa hiyo kuhakikisha wananlima mazao
mbalimbali kwa wingi na masoko ya mazo hayo yapo kwakuwa Kagera inapakana na
nchi tano ambazo ni fursa ya masoko ya mazao yanayolimwa.
|
![](https://3.bp.blogspot.com/-8eFqn3vjovY/W3NROrds_TI/AAAAAAABJzU/o-tAvpYsXp4P1VLmtvv1DHqe8KVm3qtbwCLcBGAs/s640/38820840_1920791811275870_6000996144979640320_n.jpg)
No comments:
Post a Comment