Zaidi ya
Shilingi Milioni 592.519 zimetumika katika mategenezo ya barabara 32 zenye
urefu wa kilomita 86, na ujenzi wa makaravati 20 katika barabara 14
katika kipindi cha mwezi Julai 2017/2018.
Mhandisi wa
TARURA kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara mkoani Kagera Bw.Christopher
Masunzu amebainisha hayo hivi
karibuni na kwamba Matengenezo hayo yamegawanyika katika makundi matano.
Ameyataja
makundi hayo kuwa ni Matengenezo ya kawaida (routine maintenance)
yaliyogaharimu jumla ya Shilingi Milioni 66.8 katika barabara zilizoko kata za Kanazi, Mugoma,
Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Rulenge, Kibogora, Keza, Murukurazo na
Mabawe.
Matengenezo
ya sehemu korofi (Spot improvement) katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Mbuba,
Kibimba na Nyamiaga zilizogharimu shilingi milioni 30.5
Matengezo ya
muda maalumu (periodic maintenance) yametumia shilingi milioni 150, katika kata
za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Bukiriro, Murusagamba, pamoja na Ntobeye.
Bw.Christopher Masunzu amesema matengezo mengine yalikuwa ya barabara
3 za lami zenye urefu wa kilomita moja zilizojengwa katika Mamlaka ya Mji Mdogo
Ngara na kutumika jumla ya shilingi za kitanzania Milioni 304,297,239.00.
Katika mwaka
huo wa fedha 2017/2018 TARURA wilaya ya
Ngara walifanikiwa kujenga makaravati (Culverts) yapatayo 20 katika barabara 14
katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Kabanga, Kasulo, Bukiriro Murukulazo,
Kibimba, Mugoma pamoja na Ntobeye.
Aidha,
Mhandisi huyo wa TARURA amesema Makaravati hayo yamegharimu jumla ya shilingi
Milioni 40,875,200/=; huku akitoa wito kwa wananchi kuzitunza barabara hizo
kwani zimetumika fedha nyingi ambayo ingeweza kufanya kazi nyingine za
maendeleo.
Amewaonya
wananchi wenye tabia ya kulima kwenye hifadhi ya barabara kuacha tabia hiyo
mara moja, kwani wanasababisha kuziba kwa mitaro kunakopelekea kuharibika kwa
miundombinu hiyo kwa muda mfupi hasa wakati wa mvua.
|
No comments:
Post a Comment