![]() |
Waziri Jaffo alizidi kusisitiza kuwa nia ya
Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wananpata huduma bora hasa akinamama
wajawazito katika suala la upasuaji wakati wa kujifungua sasa tatizo hilo
limefika mwisho baada ya kituo hicho kukamilika.
|
![](https://4.bp.blogspot.com/-Y7TF5kl26es/W3NIb-h9lvI/AAAAAAABJys/uCJaSWWMRwI4fVkwTn0t4YsbeAq-8W5fwCLcBGAs/s640/38829188_1920805244607860_1244552819390808064_n.jpg)
![]() |
Aidha, Waziri Jaffo aliongeza kuwa Serikali baada ya kuridhishwa na ujenzi
ulivyotekelezwa katika kituo hicho imetoa tena shilingi milioni 400 nyingine za
kujenga kituo kingine katika Halmashauri ya Wilaya Hiyo ya Biharamulo.
Pamoja na
kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Waziri Jaffo alitoa tahadhari kwa Halmashauri
hiyo kusimamia mapato ambapo alisema Biharamulo haifanyi vizuri katika
kukusanya mapato.
Pia aliagiza
kuitishwa kwa Balaza Maalum la Madiwani ili kujadili ripoti ya Tume ya uchunguzi
ilioundwa kuchunguza mapato yanavuja wapi na kama ikigundulika kuna watumishi
waliohusika wachukuliwe hatua mara moja naye apewe taarifa.
|
![](https://2.bp.blogspot.com/-zHwMLAH7Fyw/W3NIcvLfTKI/AAAAAAABJy0/KJmNWDCjeaQsMs24miNOtCulxaKQnZMfgCLcBGAs/s640/38897676_1920804941274557_2439768022307569664_n.jpg)
![]() |
Kituo cha
Nyakanazi kimekamilika ujenzi wake kwa jumla ya shilingi milioni 700 ikiwa
shilingi milioni 500 zilitolewa na Serikali kujenga majengo ya Wodi ya
akinamama na watoto, Wodi ya watoto, chumba cha kuhifadhi maiti, Nyumbambili
(Two in one) za watumishi na kukarabati chumba cha upasuaji.
Pia shilingi
milioni 200 zilitumika kununua vifaa katika kituo hicho.
Waziri Jaffo
alimaliza kwa kusema kuwa Serikali itajenga vituo vyote vya afya Wilayani
Biharamulo ili wananchi wote wapate huduma safi, pia alisema wakati Serikali ya
Awamu ya Tano inaingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 115 tu
lakini hadi sasa vimejengwa vituo 210 na tayari vituo 97 vimepewa fedha
kujengwa, hayo ni mafanikio na mapinduzi makubwa katika Sekta ya Afya.
|
No comments:
Post a Comment