Lori la Bia lapinduka Darajani Kyaka barabara Kyaka -Karagwe mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, July 02, 2018

demo-image

Lori la Bia lapinduka Darajani Kyaka barabara Kyaka -Karagwe mkoani Kagera.

.com/simgad/
IMG-20180702-WA0011
Muonekano wa  Lori lenye namba za usajili T.464 BWZ  likiwa limepinduka katika daraja la Kyaka lililopo barabara ya Kyaka –Karagwe mkoani Kagera wakati likitokea Dar es Salaam kwenda wilayani Karagwe majira ya saa 10 jioni  ambapo dreva na utingo walinusurika kifo japo walipata majeraha madogo.

Dreva wa Lori hilo Samwel Gendo licha ya kukataa kuhojiwa na waandishi wa habari alikiri kupoteza mwelekeo wakikata kona katika daraja hilo na kushindwa kulimudu, hatimaye gari kuanguka.
IMG-20180702-WA0012

IMG-20180702-WA0015
Aidha gari hilo lilikuwa na tela lake lenye namba za usajili T.898 DDL ambalo pia lilijaa kreti za bia vyote kwa pamoja vilipinduka kutokana na uzito wa mzigo ambapo kiwango cha tani hakikutajwa.

Inaelezwa baada ya ajali kutokea watu walibeba chupa za bia na kukimbia nazo majumbani hadi Jeshi la Polisi lilipofika kwa kushirikiana na Jeshi la Akiba (mgambo) kuimarisha ulinzi na usalama ambapo baadhi ya kreti za bia zilimwagikia kwenye  daraja la Kyaka barabara ya kuelekea wilayani Karagwe mkoani Kagera.
IMG-20180702-WA0013
Askari wa Jeshi la Polisi wamekutwa eneo la tukio wakilinda Usalama wa Mali hiyo na Dereva wakiwasiliana na mmiliki wa hilo gari kuweza kupata sulihisho la safari iliyoishia katika daraja la barabara ya Kyaka kwenda Karagwe.
IMG-20180702-WA0014

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *