Hospitali ya
Maweni mkoani Kigoma, Bukoba mkoani Kagera na ile ya Mkoa wa Geita zimetangazwa
na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto rasmi kuanzia
Juali 1 2018 Kuwa Hospitali za Rufaa za Mkoa.
Aidha Wizara
hiyo imepokea Hospitali 28 za Rufaa za
Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI .
Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameyabainisha hayo leo July 02,2018 wakati
alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.
“Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na
jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536,
Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada
zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri
Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo
Wizara imezipokea ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru (Arusha), Dodoma
General (Dodoma), Kitete (Tabora), Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi),
Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo (Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine
(Lindi), Maweni (Kigoma), Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke
(Dar es Salaam), Songwe, Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga
(Rukwa), Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati
(Manyara) na Bukoba (Kagera).
Waziri Ummy alisema kuwa katika mwaka wa fedha
2018/2019, Wizara imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa
miundombinu ya kipaumbele katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambako tayari
huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu kwa wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji
wa dharura hususani wakati wa ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa
wagonjwa mahututi zikiwemo za watoto wachanga .
Mnamo
Novemba 25, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa
akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) aliagiza kuwa Hospitali za Rufaa za Mikoa
zihamishiwe kwenye usimamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
No comments:
Post a Comment