Mwanafunzi wa shule ya msingi Kaniha wilaya ya
Biharamulo mkoani Kagera Masembo Sizya wa darasa la nne ametumia ubunifu wa kiakili
na kuunda mashine ya kusaga akitumia vifaa vya plastiki akiongeza nyaya za
umeme na mota ya radio.
Mwanafunzi huyo pia ameunda gari linalotembea
bila mafuta ispokuwa nishati ya umeme akionesha jinsi vijana wanavyoweza
kujikita katika ufundi wakiwezeshwa kupata vitendea kazi.
Alikuwa
katika maonesho ya wiki ya elimu kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani
Kagera,yaliyofanyika kiwilaya na kuwashangaza wadau mbalimbali waliokuwa katika
maonesho hayo na kudai serikali haina bidi kuandaa shule zenue watoto walio na
vipaji maalum.
Watoto
wengine walionesha umahili katika kuchonga , kuchora kufinyanga na kiuunda
maumbile ya sura ya nchi kupitia masomo ya stadi za kazi, jografia na saynsi
"Mwanzoni waliniita mwizi au taahila kwa kubeba na kukusanya makopo au
chupa za plastiki lakini sikukata tamaa naongeza ujuzi" Alisema mwanafunzi
huyo.
Hata hivyo Kaimu Afisa elimu idara ya msingi
wilayani Biharamulo Amosi Nyamtera amesema ili kuibua vipaji ngazi za vijiji na
hata mjini no kuwaibua watoto wengine wenya ulemavi kufundishia na kukuza
vipaji vyao.
Na-Shaaban
Ndyamukama.
No comments:
Post a Comment