Wakuu wa Shule
za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa
kuweka mikakati ya kupunguza Utoro wa Wanafunzi ili kuinua kiwango cha kufaulu
wilayani humo.
Afisa Elimu
Takwimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bw.
Zacharia Mkumbo,ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha Walimu Wakuu wa Shule
za Sekondari, kilichoandaliwa na Idara ya Elimu Sekondari kilichofanyika Shule
ya Sekondari Ngara Julai 12, 2018.
“Kama Wakuu wa Shule tujiwekee mkakati wa kukomesha utoro ili
takwimu za kufikia Machi mwaka kesho,2019 zishuke, kwa sababu hadi sasa kila
mmoja wetu anajua yuko wapi na anatakiwa kufanya nini ili kutimiza azma hiyo.”
Alisema Bw. Mkumbo.
Shule
zinazoongoza kwa utoro ni Bukiriro
yenye watoro 112, Shunga wanafunzi
80, Kibogora wanafunzi 58, Muganza wanafunzi 57,Shule nyingine ni Rusumo yenye wanafunzi 52.
Amewataka Wakuu
hao wa Shule kuwahimiza Walimu wa Madarasa, kuripoti na kuwafuatilia Wanafunzi
watoro na kuwarejesha shuleni, ili wasipoteze na kukosa haki yao ya msingi
ambayo ni elimu.
Bw. Mkumbo amesema walimu wa madarasda ni zaidi
ya wazazi kwani wana muda mrefu wa kukaa na wanafunzi; hivyo wanawajibika
kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria shuleni hadi watakapohitimu masomo yao.
Naye Kaimu Afisa
Elimu Sekondari Bw. Marton James
amewakumbusha Walimu Wakuu wakomeshe tabia ya baadhi ya walimu shuleni kwao,
wenye tabia ya kuwatukana watoto kwa madai kwamba tabia hiyo inawakatisha tamaa
Wanafunzi ,kwani hadi Machi 2018, wanafunzi wapatao 674 wameacha Shuleni na
kutokomea kusikojulikana.
Nao Walimu Wakuu
wameishukuru ofisi ya elimu sekondari kwa kuandaa kikao hicho ambacho kwao
kimekuwa cha manufaa kwani wameweza kushirikishana kimawazo; huku wakikemea
pale pasiponyooka.
|
No comments:
Post a Comment