Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rusumo.
Katika
kipindi cha robo ya tatu Idara ya Elimu Sekondari kupitia shule za Sekondari
23, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara,mkoani Kagera imepokea shilingi milioni
171,139,189.00 kwa ajili ya elimu bila malipo, katika kipindi cha Januari hadi
Machi 2018.
Kaimu Afisa
Elimu idara ya Elimu sekondari ,Bw. Marton
James, amedhihirisha hayo wakati wa kikao cha robo ya tatu, kilichofanyika
mwishoni mwa mwezi Aprili 2018, katika ukumbi wa Halmashauri.
Amechanganua
kwamba katika kipindi hicho, idara yake imepokea jumla ya shilingi milioni 25,425,297.00,
ikiwa ni fedha ya fidia ya ada kwa shule za kutwa, ambapo shilingi milioni 115,528,416.00, zimetolewa kwa ajili
ya kununua chakula kwa wanafunzi wa bweni.
“Pia tumepokea shilingi milioni 18,685,476.00,
ili zitumike kwa ajili ya uendeshaji, ambapo shilingi milioni 11,500,000.00,
tumezipokea na tumelipa wakuu wa shule za sekondari posho ya madaraka.”
Alisema Bw. James.
Kaimu huyo
wa elimu sekondari Bw.James,
ameishukuru serikali kwa kupeleka fedha ya elimu bila malipo kwa wakati, kwa
sababu hiyo shule 23 za sekondari wilayani humo, zimefanikiwa kuendesha shule
hizo kwa urahisi.
Aidha,
ameongeza kwamba idadi ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza katika mwaka 2018, imeongezeka kutoka 3288 hadi kufikia wanafunzi 3826.
Kaimu huyo
wa sekondari hakusita kutanabahisha kwamba, idara yake ina upungufu wa walimu
wa sayansi hasa wa hisabati, na wataalamu wa maabara na kwamba jumla ya
maabara 69 hazijakamilika ujenzi wake, kwani ni zimekamilika maabara 22 tu.
|
Friday, May 04, 2018

Home
HABARI
Zaidi ya Shilingi Milioni 171 za Elimu Bila Malipo zapokelewa Idara ya Elimu Sekondari wilayani Ngara.
Zaidi ya Shilingi Milioni 171 za Elimu Bila Malipo zapokelewa Idara ya Elimu Sekondari wilayani Ngara.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment