![]() |
Teknolojia
hiyo ya setilaiti inaweza kutoa intaneti yenye kasi ya Mbps 30 hadi 40,
lakini kwasababu setilaiti huudumia ndege zaidi ya moja kwa wakati mmoja, kasi
inaweza kupungua.
Lakini pia maeneo yenye bahari yanaathiri upatikanaji wa
intaneti japokuwa kasi inabaki ileile wakati ukiperuzi Facebook na Youtube.
Kama
utahitaji laivu video italazimika kuhamia kwenye mawimbi ya Ka-band.
Teknolojia
ya Ka-band inakupa intaneti yenye nguvu ndani ya ndege. Inatumia Setilaiti ya ViaSat1 ambayo kasi yake ni kubwa kwa Mbps 70 hadi 80 sawa na kasi ambayo
mtu anafurahia akiwa anatumia intaneti ya nyumbani au ofisini.
Hata hivyo
huduma hii ni ghali, inapatikana tu kwa wenye uwezo wa kuinunua. Hupatikana
zaidi kwenye ndege kubwa kama JetBlue, Virgin America na Emirates.
Kwanini
siyo kila ndege inatoa huduma ya Wi-Fi?
|
![]() |
Minara ya simu inatuma mawimbi ya redio kwenye
ndege kuwezesha Intaneti.
Wataalamu wa
anga wanaeleza kuwa kisahani kinachoshikilia antenna ni kinene na kizito; kwa
maana hiyo injini ya ndege inatumia mafuta mengi kuhimili uzito wa ziada.
Wamiliki wa ndege watatumia pesa nyingi kuwafurahisha wateja wao watapandisha
bei ya tiketi ili kufidia gharama za intaneti.
Bahati
nzuri, Wahandisi wanaendelea na mchakato wa kutengeneza antenna nyembamba,
nyepesi na yenye gharama ndogo inayoweza kutumia mafuta kidogo.
Ikiwa
watafanikiwa, watasaidia kuokoa mafuta na fedha nyingi zinazotumika kutoa
huduma hiyo.
Naamini hata
kasi ya intaneti itaboreshwa ili wasafiri wa ndege wafurahie ukuaji wa
teknolojia kwa kutazama na kuperuzi kwa uhuru mambo wayatakayo wakati wakiwa
angani.
|
No comments:
Post a Comment