Meneja wa
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Ngara (NGUWASA) Eng. Simoni Ndyamukama katikati akitoa maelezo ya huduma ya maji kwa Mkuu wa wilaya hiyo Michael Mtenjele (kushoto) sambamba na Mkurugeni wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara ,Aidan Bahama (kulia).
Mamlaka ya
Maji na Usafi wa Mazingira Ngara Mjini mkoani Kagera (NGUWASA), katika kipindi
cha robo ya tatu ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, imefanikiwa kukusanya
zaidi ya shilingi milioni 34.7 na kutumia zaidi ya shilingi milioni 35.
Meneja wa
Mamlaka ya Maji Eng. Simoni Ndyamukama,
aliyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha robo ya tatu,
kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mwishoni mwa Aprili 2018.
Eng. Ndyamukama amesema kufikia tarehe Machi, 2018,
Mamlaka imefanikiwa kuwa na wateja 2,639, na kwamba NGUWASA ina lenga kutoa
huduma ya maji kila siku, kwa wakazi wa mji wa Ngara kwa kutumia
teknolojia ya mitambo 3 ya kusukuma maji.
“Katika kipindi cha Januari hadi kufikia
Machi 2018, hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya mji wa Ngara,
ambayo ni Mubinyange, Nyamiaga, Murgwanza, Nakatunga na Buhororo, ilikuwa ni ya
wastani.” Alisema Eng. Ndyamukama.
Jumla ya
matumizi katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018 mamlaka imetumia shilingi.
35, 794,980, ambapo shilinigi milioni 24, 300,000 zimetumika kulipia gharama za
umeme wa kuendeshea mitambo.
Eng. Ndyamukama amesema kwamba, Mamlaka ya Maji
imetumia jumla ya shilingi milioni 11, 494,980, kuwalipa wafanyakazi mishahara,
kukarabati miundombinu na uendeshaji wa ofisi.
Aidha,
amesema hadi Machi, 2018, Mamlaka inadai shilingi milioni 22, 972,820.00,
ambapo Wadaiwa wakubwa ni taasisi za Serikali ambazo ni Magereza inayodaiwa
shilingi milioni 18, 180,650, na taasisi nyinginezo zanadaiwa shilingi milioni 2,
831,720.00, ambapo watumiaji wengine wanadaiwa shilingi milioni 1, 960,500.00.
Kupanda kwa
gharama za umeme wa kuendeshea mitambo ya kusukuma maji ni changamoto,
inayosababisha Mamlaka ishindwe kutekeleza majukumu yake mengine, kwani kwa
mwezi mmoja pekee gharama za ankra za umeme zinafikia wastani wa shilingi milioni
12, 000,000.00.
|
No comments:
Post a Comment