MATOKEO YA MECHI ZA LEO MAY 11, 2018.
Wenyeji GIPCO FC Mabingwa wa soka mkoani Geita wameshindwa
tena leo May 11, 2018 kuibuka na ushindi kwenye uwanja wa nyumbani wa WAJA
wakati timu hiyo iliposhukda katika dimba hilo kucheza mechi yake ya 3 ya ligi
ya Mabingwa wa Mikoa dhidi ya UNGINDONI
FC ya Dar es Salaam.
Mchezo huo
wa kundi A umemalizika kwa sare ya bila kufungana huku Mabingwa wa Soka mkoa wa
Mwanza PHANTOM FC wakiishindilia bao
2-1 NYAMONGO FC ya Mara kwenye
mchezo wa mapema kabisa saa 8 mchana.
Kwa matokeo
hayo ,PHANTOM FC wanaongoza kundi
hilo wakiwa na Point 7 za michezo 3 wakifuatiwa na KUMUYANGE FC walioshinda jana bao 3-2 dhidi ya AMBASSADOR FC ya Simiyu
–wakijikusanyia point 6 za mechi 2.
KATIKA KITUO CHA RUKWA.
Mabingwa wa
soka mkoa wa Kigoma-RED STARS wameibuka
na suhindi wa bao 1-0 dhidi ya LAELA FC
ya Rukwa katika mchezo wao wa pili wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa.
|
No comments:
Post a Comment