Wananchi
katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera wameshauriwa kutumia mifumo ya kibeki
iliyoenea nchini, ili waweze kuepuka matatizo mbalimbali yakiwemo ya fedha
bandia na kuvamiwa.
Hayo
yamesemwa na Meneja Msaidizi Kitengo cha Sarafu Benki Kuu ya Tanzania tawi la
Mwanza Bw. Ilulu said Ilulu, wakati akitoa semina ya jinsi ya kuepuka fedha
bandia Aprili 27, 2018, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Amesema
biashara ya noti bandia katika nchi ya Tanzania imepungua kwa kasi, kwa sababu
wananchi wanatambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya kifedha, iliyopo hapa
nchini.
“Tunawashauri
wananchi wote, kwamba wanapopata tatizo la kubambikiziwa noti bandia; ama kwa
makusudi au kwa bahati mbaya, watoe taarifa mara moja katika vyombo
vinavyohusika, ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.” Alisema Bw. Ilulu.
Meneja huyo
amewataka wananchi kutunza noti ili zisichakae, kwani zikidumu kwa muda mrefu,
zinasaidia kupunguza gharama za kurudufu noti mpya; fedha ambayo ingetumika
kutengeneza noti mpya inatumiaka katika shughuli za maendeleo.
Aidha,
ameonya kwamba watu waepuke tabia ya kulipwa fedha kwa keshi, kwani ni hatari,
ambazo amezitaja kuwa ni ama kuvamiwa au kupata noti bandia.
Semina hiyo
imedumu kwa siku moja na imewahusisha Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ngara.
|
No comments:
Post a Comment