Jumla ya
watoto 100 wamejitokeza kupata chanjo ya aina mbalimbali katika zahanati ya
kijiji cha Bugarama wilaya ya Ngara mkoani Kagera licha ya Mganga wa kutoa
chanjo hiyo kuwa mmoja katika Zahanati na kusababisha akina mama kusongamana wakati
wakihitaji huduma.
|
Wakiongea na
Radio Kwizera Hivi Karibuni katika Zahanati hiyo baadhi ya wazazi wenye watoto
chini ya miaka mitano waliopeleka watoto wao kupata chanjo wamesema wanapata
usumbufu mkubwa kwa sababu ya kuhudumiwa na mganga mmoja.
Aidha Mganga
Mfawidhi wa Zahanati ya Bugarama, Yudosia
Ntaramuka amesema kila siku anatoa huduma ya kuwatibu wagonjwa, wajawazito
na chanjo kwa watoto na wastani wa wagonjwa ni kati ya 30 hadi 40 kwa siku na
wanahitajika watumishi tisa kuweza kumudu wateja wanaojitokeza.
|
Baadhi ya
wanawake waliokuwa katika Zahanati hiyo walisema wanahangaika sana kupata
huduma kutokana na msululu au msongamano wa wanaohitaji huduma.
Hata hivyo
Mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama Jaafari
Saidi amesema Serikali ya halmashauri ya wilaya hiyo ijaribu kuongeza
watumishi kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya kwani zahanati hiyo
inahudumia vijiji vya Bugarama na Rwinyana.
Habari Na Radio Kwizera.
|
No comments:
Post a Comment