![]() |
Picha ya Pamoja ya Waandishi wa Habari Mkoani Kagera wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mei 3,2018 mkoani Humo.
Na:
Sylvester Rapahel
Waandishi wa Habari Mkoani Kagera wamekumbushwa kwenda kwa wananchi katika ngazi za chini kabisa hasa vijijini kuona matatizo ya wananchi na kuyaibua kwa kuandika habari zao zitakazolenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao na kuwatoa sehemu moja na kupiga hatua ya maendeleo kuliko kuandika habari za mijini tu ambazo zimezoeleka. |
![]() |
Katika
hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa
Wilaya alivipongeza vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera kwa
kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo ya mkoa kwa kuandika habari ambazo
zinaelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuinua uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.
|
![]() |
Aidha, Mkuu
wa Wilaya katika hotuba yake aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa Serikali
Mkoani Kagera itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari ili vitimize
wajibu wake pia Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili wananchi
ambao ni walaji wapate habari sahihi na zenye uhakika.
Katika
Maadhimisho hayo yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Kagera (
KPC) pia walialikwa wadau mbalimbali ambao walishirikiana na waandishi wa
Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari kujadili na kuchambua mada isemayo “Uhuru wa Habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa maendeleo ya Mkoa.”
Wadau
wakichangia mada hiyo waliwashauri Waandishi wa Habari kuhakikisha wanaandika
habari zenye vyanzo vyenye uhakika na zenye maslahi mapana na jamii ili
kubadili mtazamo wa jamii kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya maendeleo.
Pia
Waandishi wa Habari walishauriwa kuhakikisha wanazama chini katika jamii
kuandika habari za wananchi wa kawaida au kuandaa vipindi ambavyo vinawagusa
wananchi wa chini kabisa ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika maisha
yao kwa kuelimishwa kupitia vyombo vya habari.
|

![]() |
Kwa sasa
Mkoa wa Kagera unavyo Vituo vya Redio vipatavyo 9,ambavyo ni Kasibante FM, Fadeco Redio, Karagwe FM , Shinuz FM, KCR FM,
Vision FM, Kwizera FM, Bukoba FM na Redio Mbiu. Pamoja na Redio
nyingine nyingi ambazo zinasikika katika Mkoa wa Kagera zikirusha matangazo
yake kutoka nje ya mkoa.
Pamoja na
Redio kuna Magazeti, Mitandao ya Kijamii, Cable TV, ambavyo vinautangaza mkoa
wetu wa Kagera na kuwapasha wananchi wake kupitia Waandishi wa habari ambao
wametapakaa mkoa mzima wakiandika habari mbalimbali za michezo, kuichumi,
kijamii, Elimu, Utalii, Uwekezaji na nyinginezo nyingi.
Siku ya Mei
3 ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari Duniani. Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani huongeza ufahamu
wa umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuikumbusha Serikali wajibu wake wa
kuheshimu na kuhakikisha haki ya uhuru wa kujieleza inaheshimika chini ya Ibara
ya 19 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu la 1948. Pia katika Siku hiyo
Hukumbukwa Waandishi waliotangulia Mbele za Haki.
|
No comments:
Post a Comment