![]() |
Mganga wa jadi akimpigia ramli mwandishi wa kitabu
hiki (hayuko pichani) baada ya kutoa Shs. 2,000 akitaka amwangalizie kwanini
'mkewe' (askari mmoja wa kike aliyekwenda naye wakiwa kikazi) alikuwa hazai. Mganga alisema mwanamke huyo alikuwa 'amelogwa' na mwanamke aliyetaka kuolewa na mwandishi halafu yeye akamkataa, ambapo kiuhalisia hakuwepo mwanamke wa aina hiyo na hata huyo aliyekwenda naye walikutana kikazi na hawakuwa wakifahamiana kabisa. |
![]() |
Mtoto Baraka Cosmas akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya baada ya kukatwa kitanga cha mkono Machi 7, 2015. |
![]() |
Mwandishi Daniel Mbega (mwenye fulana nyekundu na kofia ya sweta) akiwa sambamba na wanausalama katika nyumba ambamo Baraka Cosmas alikatwa kitanga cha mkono Machi 7, 2015. |
![]() |
Mtuhumiwa Sajenti Kalinga Malonji akiwa chini ya
ulinzi baada ya kukishusha kiganja cha Baraka Cosmas kwenye mti nyumbani kwake
kijijini Hanseketwa, Mbozi siku ya Jumapili, Aprili 26, 2015. Sajenti tayari amehukumiwa miaka nane jela na wenzake wamehukumiwa vifungo vya hadi miaka 20 Jela. |
![]() |
Mwandishi Daniel Mbega, akiwa kwa mganga huko
Kachwamba, wilayani Chato wakati akifanya uchunguzi wa mauaji ya Albino.
Aidha,
amesema kwamba, katika uchunguzi wake huo alishiriki pia kikamilifu katika misako
mbalimbali ya wahalifu walioshiriki kwenye matukio hayo na kushuhudia namna
vyombo vya ulinzi na usalama vinavyotenda kazi.
Kunusurika
kifo kwa ajali ama kuzingirwa na baadhi ya wananchi ni moja ya hatari
alizokumbana nazo wakati wa uchunguzi wake, huku akisafiri umbali wa zaidi ya
kilometa 40,000 katika kipindi hicho.
“Wakati
mwingine nilikosa usingizi hata kwa siku tano mfululizo, nililazimika kusafiri
mchana na usiku katika mazingira mengi hatarishi nikikusanya habari,” alisema.
Akaongeza:
“Haikuwa kazi rahisi kuweza kufanya mahojiano na waganga wa jadi, achilia mbali
wachawi ambao baadhi yao waliamua kujiweka wazi na kueleza mambo yanayotendeka
katika ulimwengu wa giza na jinsi yanavyohusiana na mauaji ya wenye ualbino.”
Alisema
katika uchunguzi huo alikumbana na mambo mengi ya ajabu ikiwa ni pamoja na
kushika matunguli, pembe zinazofoka damu, damu na maiti, mifupa inayodhaniwa
kuwa ya binadamu na mambo mengine kadha wa kadha.
Aidha,
alisema kwamba, alizungumza pia na wanamichezo, baadhi ya viongozi wa dini
ambao nao wanatumia nguvu za giza ambapo waganga walieleza jinsi nao
wanavyoshiriki katika matukio hayo ya mauaji ya wenye ualbino.
“Ni mtandao
mpana sana, siyo Tanzania tu, bali hata katika nchi jirani za Kenya, Malawi,
Burundi, Msumbiji, Afrika Kusini na Swaziland… naamini kkitabu hiki kitaiamsha
jamii na kubadilisha mitazamo ya watu mara watakapojifunza yale niliyoyakusanya
kutoka kwa vinywa vya wahusika wenyewe,” amesema na kusisitiza kwamba amepanga
kitabu hicho kiwwe mtaani mwishoni mwa mwezi Septemba ikiwa atapata msaada wa
kufanikisha uchapaji.
|
No comments:
Post a Comment