![]() |
Simba SC.
Kipigo cha
2-0 ilichochezea Yanga SC kutoka kwa Tanzania Prisons, kimeivua rasmi Ubingwa
wa VPL iliyoubeba msimu wa 2016/2017 ambao sasa unakwenda mitaa ya Msimbazi kwa Simba SC ambayo hata
ikipoteza mechi zake zote (3) bado hakuna timu ambayo itaweza kuifikia.
Simba SC
inaongoza Ligi msimu huu 2017/2018 ikiwa na pointi 65 baada ya kucheza mechi
27, imebakiza mechi tatu kabla ya msimu wa ligi haujaisha.
Yanga SC
ambayo ilikuwa Bingwa mtetezi inaendelea kubaki na pointi zake 48 baada ya
kuheza mechi 25 na kubakiza mihezo mitano (5).
Endapo Yanga
SC itashinda michezo yote mitano iliyosalia itafikisha pointi 63, ambazo ni
pointi mbili nyuma ya Simba SC.
|
![]() |
Yanga SC.
Matokeo haya
pia yanamaanisha Yanga CS hawatashiriki michuano ya Afrika mwakani, kwani
tayari wametolewa pia na kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC) katika hatua ya Robo Fainali
tu.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu May 11,2018, bao pekee la Vincent Philipo dakika ya 45 na ushei limeipa Mbao FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa CCM Kirumba mjiniu Mwanza. Kwa ushindi huo, Mbao FC inafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati Ndanda FC inabaki nafasi ya 15 kwa pointi zake 23 za mechi 28 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo timu mbili zitashuka wiki mbili zijazo. |
No comments:
Post a Comment