![]() |
Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Wanawake wa CCM Kata ya Rusumo wilayani
Ngara mkoani Kagera wakitoa burudani wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la
Ngara mkoani Kagera Alex Gashaza Jana
May 6,2018.
|
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe. Alex Gashaza amefanya
mkutano wa hadhara na Wananchi wa Rusumo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari
Kabulanzwili ambapo alihimiza Miradi mbalimbali ya maendeleo itolewe
taarifa na kuwashirikishaViongozi na Wananchi ili itekelezwe kwa ufanisi zaidi.
Ameahidi kuendelea kuizungumzia Bungeni miradi ya maendeleo ambayo bado
haijakamilika ikiwemo huduma ya maji safi na salama na wananchi wa Kata ya
Rusumo kupewa kipaumbele kwenye mradi wa maporomoko ya Rusumo.
Aidha,Mhe Gashaza,amesema kuwa wilaya ya Ngara itapatiwa Shilingi
Milioni 200 kwa ajili ya Utekelezaji wa mradi wa Maji ambapo zitatumika katika
ujenzi wa Matenki mawili makubwa katika mlima Shunga ili kusambaza maji katika
wilayani hiyo.
Picha/Habari Na –Radio Kwizera Ngara.
|

![]() |
Wana CCM na Wananchi wakifatilia mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Ngara
mkoani Kagera Alex Gashaza Jana May
6,2018.
|



![]() |
Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera
Alex Gashaza.
|

No comments:
Post a Comment