Walimu Halmashauri ya Mji wa Kasulu waanza Mgomo baridi Kudai Stahiki zao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 08, 2018

Walimu Halmashauri ya Mji wa Kasulu waanza Mgomo baridi Kudai Stahiki zao.

 Walimu waliohamishwa kutoka shule za sekondari kwenda masingi katika Halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma, wameazimia kuendesha mgomo Baridi na kutofika kwenye vituo vyao walivyopangiwa, mpaka watakapopewa stahiki zao zote

Maamuzi hayo yamefikiwa hii May 7,2018 wakiwa nje ya ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bi. Fatina Laayi wakidai kupata mwafaka juu ya malipo yao ya uhamisho ili waweze kuwajibika katika shule walizopangiwa.
Walimu hao wameiambia Radio Kwizera kuwa wamefuatilia zaidi ya miezi mitatu sasa tangu kutolewa kwa agizo hilo lakini mpaka sasa hawajapatiwa stahiki zao huku nao wakiahidi kutofika katika vituo walivyopangiwa mpaka stahiki zao zitakapolipwa.
Katibu wa Chama cha walimu (CWT) wilayani Kasulu Mwl. Buchumi Felister Nkayamba, amesema msimamo wa chama cha walimu ni kuitaka halmashauri hiyo kuwalipa walimu stahiki zao kama maelekezo ya Rais yanavyoelekeza.

Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bi. Fatina Laayi, alipoulizwa kuhusu malalamiko ya walimu hao amesema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo ambapo radio kwizera inaendelea kufuatilia kwa ajili ya kupata majib.

 Na –Radio Kwizera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad