![]() |
Rais Dkt.
John Magufuli amewataka Viongozi wa Serikali kuacha kutoza ushuru kwa wananchi
wanaosafirisha bidhaa na mazao ambayo hayajafika uzito wa tani moja,
kwakuwa bunge mwaka 2017 lilipitisha sheria ya kufuta tozo zaidi ya 87 katika
sekta ya kilimo.
Rais
Magufuli alisema hayo jana Mei 05, 2018, katika sherehe za uzinduzi wa daraja
Magufuli lililopo katika mto Kilombero mkoani Morogoro, na kusema kuwa jukumu
la Serikali ya awamu ya tano ni kutatua kero za Wananchi hasa wakulima na kama
Rais wa nchi anazijua kero hizo kwasababu amekua kiongozi wa serikali kwa zaidi
ya miaka 20.
“Nataka
nitoe wito kwa viongozi, ukimuona mtu amebeba magunia 10 ya mpunga maana yake
hayajafika tani moja, mpishe wala usimuangalie mwache asafirisha mizigo yake,
nataka viongozi wenzangu mnielewe nilizunguka Tanzania nzima kuomba kura kwa
ajili ya kuwatetea wananchi, ninafahamu kero za wananchi, wewe kama ni mtoza
ushuru nenda ukalime ukajitoze ushuru mwenyewe” alisema Rais Magufuli.
Rais Dkt.
Magufuli ameongeza kuwa serikali haiwezi kuwa kikwazo cha maendeleo kwa
wananchi na kuongeza kuwa anataka daraja hilo liwanufaishe wananchi wa Morogoro
na kuwasihi wakulima kusafirisha bidhaa chini ya tani moja kama wanataka
kuepuka kutozwa ushuru.
Daraja la
Magufuli lipo katika mto Kilombero, barabara kuu ya Kidatu Ifakara na
lina.
|
Monday, May 07, 2018

Rais Magufuli -Marufuku Viongozi wanaowatoza Ushuru wa Mazao Wananchi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment