Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiangalia Kimondo cha
Mbozi alipotembelea kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe
jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo
duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni
cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na
mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur
0.01% na Phosphorus 0.11.
Na Hamza Temba-WMU-Songwe
.............................. .............................. ..............
Mkoa
wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau
wengine wa uhifadhi na maendeleo utafanya maadhimisho ya siku ya Kimondo
cha Mbozi kwa mara ya kwanza katika historia kwenye Kijiji cha Ndolezi
Kata ya Mlangali, wilayani Mbozi kuanzia Juni 28 hadi 30 mwaka huu .
Maadhimisho
hayo yataenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vimondo duniani ambayo
yaliazimiwa kufanyika Juni 30 kila mwaka na kikao cha Umoja wa Mataifa
cha tarehe 6 Desemba, 2016.
Pamoja
na mambo mengine, kikao hicho pia kiliazimia tarehe hiyo kuwa siku ya
kuelimisha umma kuhusu elimu ya anga na mafanikio ya tafiti mbalimbali yaliyopat ikana
kuhusu elimu hiyo, kutambua juhudi zilizofanyika, kuweka sheria za
kimataifa na kutoa tahadhari juu ya athari zinazoweza kutokea endapo
dunia itafanya uharibifu juu ya anga.
Taarifa
hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi na Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Herman Tesha wakati akiwasilisha taarifa
ya maandalizi ya maadhimisho hayo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ambaye alitembelea kituo hicho kwa ajili ya
kukagua shughuli za maandalizi.
Amesema
lengo la maadhimisho hayo ni kutangaza Kimondo kama kivutio muhimu cha
utalii mkoani Songwe pamoja na vivutio vingine vya mkoa huo kwa ujumla
ili kutoa fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya utalii mkoani humo.
Amesema
maadhimisho hayo yataenda sambamba na kongamano la uwekezaji na sayansi
ya vimondo, maonesho ya malikale, maonesho ya kiutamaduni, mashindano
ya riadha (Kimondo Marathon), mashindano ya netiboli na mpira wa miguu
(Kimondo Ligi).
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
amesema Serikali kupitia Wizara yake itashiriki kikamilifu katika
maadhimisho hayo kwa kushirikiana na mkoa wa Songwe na wadau wengine ili
kuhakikisha kivutio hicho cha Kimondo kinajulikana zaidi ndani na nje
ya nchi na hatimaye kiongeze idadi ya watalii na mapato.
Amesema
wizara yake ina mkakati maalum wa kuimarisha kituo hicho cha utalii
ambapo hivi sasa imeshajenga kituo maalum cha taarifa ambacho
kimegharimu zaidi ya Shilingi milioni 400 za Kitanzania.
Aidha,
amesema kupitia mkakati mpya wa wizara wa kuimarisha na kuvijengea
uwezo vituo vya malikale nchini kwa kuzishirikisha taasisi za uhifadhi
wa wanyamapori na misitu, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa
litashirikiana na kituo hicho kwa kuimarisha miundombinu pamoja na
utangazaji.
Nao
wananchi wa kijiji cha Ndolezi wakizungumza kwa nyakati tofauti
hawakusita kuonyesha furaha zao kuhusu maendeleo ya eneo hilo na kuahidi
kutoa ushirikiano kwa Serikali katika mipango na miradi mbalimbali
itakayoanzishwa katika eneo hilo kwa faida ya pande zote mbili.
Katika hatua nyingine, baada ya kuhitimishwa kwa ratiba za Mwenge wa Uhuru wilayani Mbozi, wakimbiza Mwenge Kitaifa walilazimika kutumia fursa ya uwepo wao wilayani humo kwenda kutalii kwenye kivutio cha Kimondo wakati wa usiku wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga.
Katika hatua nyingine, baada ya kuhitimishwa kwa ratiba za Mwenge wa Uhuru wilayani Mbozi, wakimbiza Mwenge Kitaifa walilazimika kutumia fursa ya uwepo wao wilayani humo kwenda kutalii kwenye kivutio cha Kimondo wakati wa usiku wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga.
Kimondo
cha Mbozi kilianguka mwaka 1840 kutoka kwenye obiti yake huko angani
huku kikikadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma
90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Kimomdo hicho ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na cha nane duniani
kati ya vimondo 600 vilivyodondoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, sifa
yake kubwa ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua kali.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua mpaka wa eneo la
kituo cha kimondo na vijiji jirani alipotembelea kituo hicho cha
utalii katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana
kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo
duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni
cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na
mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur
0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua kituo cha
taarifa cha Kimondo cha Mbozi alipotembelea kituo hicho cha utalii
katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili
ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani
yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili
kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na
mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur
0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya
watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha kimondo katika
kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Nyuma yao ni
jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake umekamilika.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha
kimondo katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana.
Nyuma yao ni jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake
umekamilika. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na
kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%,
Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (nyuma kulia) akiwa
kwenye picha ya pamoja na Wakimbiza Mwenge kitaifa, Mkuu wa Wilaya ya
Mbozi, Ernest Palingo (kushoto) na waratibu wa Mwenge mkoa wa Songwe
mbele ya Kimondo cha Mbozi katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi
mkoani Songwe jana usiku baada ya shughuli za Mwenge. Kimondo hicho ni
cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na
mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur
0.01% na Phosphorus 0.11.
No comments:
Post a Comment