Muonekano wa
Daraja la KWATAMARA lililokatika kutokana baada ya maji mengi kushidwa kupita
katika matundu ya daraja hilo na kupita juu. Daraja hilo lipo katika Kata ya
Bulega wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Wakazi wa kata ya Bulega wilaya ya Bukombe Mkoa wa
Geita wameiomba Serikali kuwajengea daraja la KWATAMARA ililokatika hivi karibuni na kusababisha bei za vinywaji
na usafiri na kupanda hali inayowapa shida hasa wa kipato cha chini.
|
Wakizungumza
na Radio Kwizera baadhi yao Mashashi Mwenda, Pendo Makoye na Leonard
Malimi wamesema kutokana na mvua
iliyonyesha hivi karibuni katika kata hiyo ilisababisha daraja hilo kukatika na
kukata mawasiliano baada ya daraja hilo kusombwa na maji hali ambayo imesababisha bei ya soda 1 kupanda
kufikia sh.700 huku bei ya usafiri ikifikia shilingi elfu 6 badala ya shilingi
elfu 3 kufika makao makuu ya wilaya hiyo.
Hata hivyo
wameiomba Serikali kuwatengenezea barabara hiyo ili kurahisisha shughuli za
usafirishaji wa bidhaa kuzifikisha katika soko la BULEGA lililopo katika kata hiyo.
|
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe MHE. DOTTO MASHAKA
BITEKO amewataka Wananchi kuwa wavumilivu na kwamba amefanya mazungumzo na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAG iliyopo wilayani humo kwa lengo
la kuwasaidia wananchi kuwatengenezea barabara hiyo na kwamba tayari wamekwisha
kufika eneo hilo kwa ajiri ya utafiti wa awali kabla ya kuanza ujenzi.
Radio Kwizera.
|
No comments:
Post a Comment