Mbunge wa
Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka
Biteko akihutubia mamia ya wananchi katika Kijiji cha Kilimahewa kilichopo
katika kata ya Bulangwa wakati wa ziara za kijimbo hivi karibuni.
Picha Zote Na Mathias Canal.
Baadhi ya
wananchi katika Kijiji cha Kilimahewa kilichopo katika kata ya Bulangwa wakifatilia
hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa
Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa ziara za kijimbo hivi karibuni.
Na Mathias
Canal, Bukombe-Geita
Mbunge wa
Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka
Biteko ameendelea kutekeleza agizo la WaziriMkuu Mhe Kassim Majaliwa alilolitoa
2 Aprili 2018 wakati wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka
2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita Katika sherehe hizo zilizonakshiwa na
Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ambayo ni ‘Elimu ni ufunguo wa
maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
Waziri Mkuu
aliwagiza viongozi wa mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo
inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari
wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwani miongoni mwa
sababu zinazopelekea wanafunzi kutoelimika ipasavyo ni pamoja na utoro shuleni.
Kupitia
agizo hilo Mhe Biteko amechangia mabati 100 geji 28 yenye thamani ya Sh 2.6
milioni kwa ajili ya ukamilishaji wa kupaua vyumba vya madarasa katika shule ya
sekondari Azimio Wilayani Bukombe ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa wanafunzi kuwa
na maeneo bora ya kusomea.
Mara baada
ya uzinduzi wa Mwenge huo wa Uhuru 2 Aprili 2018 kabla ya kuelekea Mjini Dodoma
kwa ajili ya shughuli za Bunge zilizoanza 3 Aprili 2018 Mhe Doto Biteko alizuru
Kijiji cha Nampalahala kilichopo Kata ya Busonzo na kujionea jinsi ujenzi wa
maabara unavyoendelea ambapo pia alichangia matofali 10,000 kwa ajili ya ukamilishaji Wa vyumba vya
maabara ili kurahisisha uanzishaji wa shule ya sekondari wa Kata ya Busonzo
wilayani Bukombe.
Akihutubia
mamia ya wananchi waliojitokeza juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Kilimahewa kilichopo katika kata ya Bulangwa, Mhe Biteko
alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli,
imedhamiria kuboresha elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia Elimu ya Awali
hadi Elimu ya Juu hivyo wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kwa maendeleo ya
wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.
Alisisitiza
kuwa serikali imeweka mkakati wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote nchini
kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo jukumu la wazazi ni kuwapeleka
watoto shule ili kunufaika na matunda ya serikali katika utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya mwaja 2015-2020.
Aliongeza
kuwa wananchi wanapaswa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho chama
pekee nchini kinachoshughulika na matatizo ya wananchi ikiwemo kuboresha
shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuboresha elimu, afya, miundombinu na
huduma zingine zikiwemo upatikanaji wa maji.
No comments:
Post a Comment