Mshambuliaji
Diego Costa akiinua mkono wake juu kushangilia baada ya kuifungia bao pekee
Atletico Madrid dakika ya 45 na ushei katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal
usiku May 3, 2018 kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid, Hispania.
Ulikuwa ni
mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Europa League na Atletico Madrid inaingia
fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa
kwanza London wiki iliyopita na itamenyana na Olympique Marseille
iliyoitoa Red Bull Salzburg ya Austria kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda
2-0 Ufaransa na kufungwa 2-1 ndani ya dakika 120 Wals-Siezenheim. |
No comments:
Post a Comment