Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilayani ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amepiga marufu matumizi ya daraja
linalounganisha kijiji cha Bugarama kilichoko katika tarafa ya Rulenge, na
kijiji cha Muruyungu kilichoko nchini Burundi, mpaka makubaliano rasmi
yatakapofikiwa.
Mwenyekiti
huyo Lt. Col. Mntenjele amefikia
uamuzi huo hivi Karibuni baada ya wakandarasi wa Burundi kujenga daraja hilo
bila ridhaa ya ujenzi wa daraja hilo kati ya Tanzania na Burundi.
“Matumizi ya daraja hili ni marufuku kwa
pande zote mbili; hakikisheni halitumiki, tukikuta linatumika pande zote mbili
mtawajibika.” Alisema Lt. Col.
Mntenjele.
Amesema
kujenga daraja hilo bila ridhaa ya pande mbili ni kinyume cha taratibu za
ujirani mwema, kwani mipaka rasmi inajulikana, ambayo ameitaja kuwa ni Rusumo, Kabanga na Murusagamba.
Amesema
daraja hilo si tatizo tu kwa kuvusha magendo na kuingiza wahamiaji haramu tu,
bali pia linaikosesha serikali mapato kwa kupitisha vitu kinyemela.
Aidha,
amesistiza kwamba kilichopigwa marufuku ni matumizi ya daraja na siyo ujirani
mwema, hivyo, shuguli nyingine zote ziendelee kama kawaida.
Mwenyekiti
huyo wa kamati ya ulinzi na usalama Lt.
Col. Mntenjele ameabatana na wajumbe wote wa kamati hiyo kukagua daraja
hilo lililojengwa na Burundi bila ya ridhaa ya upande wa Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment