Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack.
Serikali ya Kata ya Nsalala, Tarafa ya Itwangi, mkoani Shinyanga vijijini
imetunga sheria ndogo ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa kumtaka mtu
yeyote anayetaka kuoa ama kuozesha kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.
Lengo la sheria hiyo ni ili
kujiridhisha kuwa anayeolewa siyo mwanafunzi au msichana chini ya umri wa miaka
18.
Hayo
yalibainishwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsalala, Sandeko
Machungo kwenye mkutano maalum wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia
ndani ya jamii ulioandaliwa na Shirika la Kivulini linalotetea haki za watoto
na wanawake kwa ufadhili wa Oxfam la Uingereza.
Alisema
viongozi wa kijiji wamepata elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na ndiyo maana
wakaona watunge sheria hiyo ndogo kijijini hapo ili kuzuia wananchi kuoa ama
kuozesha bila ya kutoa taarifa kwenye uongozi huo kwa lengo la kutokomeza
tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
“Tumeshatunga
sheria kijijini hapa kwamba hakuna mwananchi kuoa au kuozesha bila kuuona
uongozi wa kijiji, sasa tunafuatilia taarifa za mtu anayetaka kuoa au kuoza ili
kuhakikisha wanaoolewa wamefikisha umri wa miaka 18 na kuhakikisha kuwa siyo
mwanafunzi kwa kuangalia vyeti vya kuzaliwa ama kadi ya kliniki ndipo tutatoa
ruhusa,” alisema Machungo.
Alibainisha
kuwa sheria hiyo waliitunga mwaka jana na tayari wananchi wamekuwa wakifanya
hivyo na tangu ianze sasa hakuna shangamoto tena za ndoa za utotoni katika eneo
lake wala mimba za wanafunzi.
“Kila
mwananchi amekuwa mlinzi wa mwenzake na atakayebainika kwenda kinyume cha
sheria hii, uongozi wa kijiji utamshughulikia.
Naye Kaimu
Afisa wa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Shinyanga Vijijini, Aisha Omari
aliipongeza serikali ya kijiji hicho kwa kutunga sheria hiyo ndogo na kutoa
wito kwa vijiji vingine nchini kuiga mfano huo ili kutokomeza ndoa na mimba za
utotoni.
|
Thursday, April 12, 2018
Serikali: Marufuku Kuoa, Kuolewa Bila Kutoa Taarifa.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment