Haya ndiyo matokeo ya Mechi zote za
VPL zilizopigwa April 11, 2018.
Timu ya soka
ya Majimaji ambayo ilikuwa ikikamata mkia katika msimamo wa ligi, leo ikiwa
ugenini, imefanya maajabu kwa kuitandika Stand United mabao 3-1 katika mchezo
wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Kambarage, Shinyanga.
Katika
mchezo huo, mabao ya Majimaji yamefungwa na Peter Mapunda, aliyefunga mabao mawili, na lingine likifungwa na Lucas Kikoti huku bao la Stand United likifungwa
na Tariq Seif.
Matokeo hayo
yanaifanya Majimaji FC kufikisha pointi 19 na kupanda hadi nafasi ya 15
ikiiacha Njombe Mji yenye pointi 18 mkiani, wakati Stand United ikiwa nafasi ya
11 ikiwa na pointi 25.
Katika
viwanja vingine, Mwadui FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC
kwenye dimba la Mwadui Complex, mkoani Shinyanga.
Mabao ya
Mwadui yamefungwa na Salim Hamis na Awadh Juma, huku bao la Lipuli
likifungwa na Zawadi Mauya.
Jijini Mbeya
Tanzania Prisons wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine
baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar.
Wageni
Kagera Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Atupele Green mnamo dakika ya 3 ya mchezo na ikabidi wenyeji
Prisons wasubiri mpaka dakika ya 83 ili kusawazisha kupitia nyota wao Mohamed Rashid.
Mbao FC kwa
upande wake baada ya kukosa ushindi kwenye mechi saba mfululizo za ligi hiyo, imeibuka
na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Njombe Mji, mchezo ukipigwa dimba la CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Mabao ya
Mbao yamefungwa na David Mwasa na Rajesh Kotecha, huku bao la Njombe
waliokuwa wa kwanza kufunga, likitiwa nyavuni na David Obash.
|
Raundi ya 24
itakamilika Alhamisi ya Aprili 12, 2018 kwa michezo minne ambapo Mtibwa Sugar
baada ya kupoteza kwa Simba bao 1-0 , watawakaribisha Ndanda FC katika Dimba
la Manungu Complex Morogoro.
Katika
viwanja vingine Stand United watapambana na Majimaji FC katika dimba la
Kambarage Shinyanga, vinara Simba watawakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam na Ruvu Shooting watajaribu kuendeleza mtindo wa
kupapasa dhidi ya Azam FC.
|
No comments:
Post a Comment