Na:
Sylvester Raphael -Kagera.
Mwenge wa Uhuru 2018 unaendelea na mbio zake Mkoani Kagera ambapo tayari Mwenge huo umekimbizwa katika Halmashauri 7 za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi , Kyerwa ,Karagwe na sasa wilaya ya Ngara leo April 14,2018 ikiwa ni kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Kagera, aidha, tayari miradi zaidi ya 44 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 6,309,492,560.70 imetembelewa, kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charles Kabeho Akimkabidhi Mzee Kitambulisho cha Matibabu Katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Mugana wilayani Missenyi mkoani Kagera. |
Akito ujumbe
wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charles F.
Kabeho katika Halamashauri za Wilaya ambazo tayari zimepitiwa na Mwenge wa
Uhuru aliwasistiza Wananchi kuwekeza katika Elimu kwa watoto wao ili
kuhakikisha watoto hao wanapata Elimu bora kwa manuaa ya taifa na mkoa wa
Kagera hapo baadae.
Kiongozi
huyo wa Mbio za Mwenge aliongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao
wanapata chakula shuleni kulingana na Waraka wa Serikali unavyoelekeza.
Pia
Wazazi wanatakiwa kuwanunulia watoto wao sare za shule, kuwalipia nauli za
kwenda shule na kuhakikisha watoto wana vifaa vyote vya shule kama madaftari na
kalamu.
Katika Hatua
nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge aliwasisitiza wananchi wa mkoa wa Kagera
kuachana na upikaji wa gongo na kusisitiza kuwa gongo ni mojawapo ya dawa za
kulevya ambazo hazistahili kutumika katika jamii.
|
Pongezi, pia
aliupongeza mkoa kwa kupambana na utoro wa wanafunzi shuleni kwamba mkoa huu
unajithidi kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo yao shuleni lakini
alisisitiza uongozi wa Mkoa kuongeza juhudi ili kufuta suala la utoro shuleni.
Mwenge wa
Uhuru ulipokelewa Mkoani Kagera Aprili 8, 2018 na tayari umekimbizwa katika
Halmashauri za Wilaya za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi, Kyerwa
,Karagwe na sasa unakimbizwa Wilayani Ngara leo April 14, 2018.
Aidha,
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa kesho April 15, 2018 katika Halmashur ya Biharamulo na utakabidhiwa Mkoa wa Kigoma
tarehe 16 Aprili, 2018.
|
No comments:
Post a Comment